WANANDOA NA VIJANA MNAOTAFUTA WACHUMBA JIFUNZENI JAMBO KWA HAWA WATU. ____________________________________

 SOMO: WANANDOA NA VIJANA MNAOTAFUTA WACHUMBA JIFUNZENI JAMBO KWA HAWA WATU.

____________________________________


Picha ya kushoto ni Kijana Jean-Pierre Adams aliyezaliwa tarehe 10, Machi 1948 katika mji wa Dakar Senegal na kisha kupewa Uraia wa Ufaransa enzi zile za Ukoloni.


Akiwa Ufaransa aliingia kwenye fani ya mpira wa miguu na kuitumikia timu ya Taifa ya ufaransa, Pia alicheza katika timu mbalimbali zikiwemo Nemes, Nice, PSG n.k. 


Picha ya kulia ni mwanamama mrembo Bernadette, mke wa Jean Adams aliyefunga nae ndoa April 1969 na kufanikiwa kupata watoto wawili wa kiume; Frederic (1967) na Laurent (1969).


Mwaka 1982, bwana Jean Pierre aliumia goti akiwa uwanjani na ikamlazimu kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Édouard Herriot jijini Lyon.


Wakati anajiandaa kufanyiwa upasuaji, madaktari walifanya kosa la kiufundi wakamchoma dawa nyingi ya usingizi ambayo ilimsababishia kuzimia (coma) kunzia mwaka huo mpaka leo.


Jitihada za kumuokoa Bw. Pierre kutoka kwenye coma zilipogonga mwamba Mkewe; Bi  Bernadette aliamua kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani akiwa katika hali hiyo ya coma.


Kwa sasa Bwana Jean-Pierre ana miaka 72 ( 1948-2020) lakini pia mkewe naye amezeeka licha ya kwamba ameendelea kumhudumia mumewe ambaye anapumua bila mashine kwa miaka 38 huku akiwa amelala usingizi.


Bi Bernadette ameishi kwa matumaini makubwa ya kwamba; ipo siku mumewe ataamka, lakini pia ameweka wazi kuwa hata kama hatoamka, ni vyema Mwenyezi Mungu amchukue mumewe huyo kabla yake kwa sababu ikiwa yeye atamtangulia basi mumewe kipenzi atakosa mtu wa kumuhudumia.


Licha ya Bw. Pierre kufanya Uchaguzi mzuri katika kuoa, kwangu mimi huyu mama ndiye shujaa wa hii ndoa, aliumbwa na moyo wa pekee ambao ni nadra kuupata kwa kizazi hiki cha "dotcom".


Aliamua kuuweka usichana wake rehani kwa miaka 38 akiishi na mtu aliyezimia bila kumkatia tamaa mpaka uzeeni, Fikiria mateso ya kihisia, kimwili, kiuchumi na kijamii anayopitia huyu mama. Kule kwetu Mara huwa tunawaita kwa usemi "Ono mokari mosacha!"


Eee Mungu tenda miujiza kwa Bw. Pierre ili huyu mama avune matunda ya uvumilivu wake.

Pia  Mungu murehemu huyu Mama kwa moyo wa ajabu alio nao.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form